BIMA YA NYUMBA / MALI: MASWALI 5 KABLA YA KUKATA
Nani anaweza kukatia Nyumba au Mali zake Bima?
Ni mtu ambaye ni mmiliki kisheria wa Nyumba hiyo au Mali hizo na ambaye kama majanga yakitokea yeye ndio atakayepata hasara za kifedha. Mali zinaweza kuwa vitu binafsi au mali za mfanyabiashara mfano wafanyabiashara (maduka yao), n,k.
Je nitanufaikaje?
Bima itakupatia fidia dhidi ya hasara au uharibifu utokanao na:
- Majanga ya Moto, mfano kama masoko yaliyowahi kuungua Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, n.k.
- Majanga ya Mafuriko
- Majanga ya Tetemeko la Ardhi, mfano yaliyowahi kutokea Kanda ya Ziwa, n.k.
- Majanga ya Upepo Mkali na Kimbunga.
- Majanga ya kudondokewa na vitu mbalimbali.
- Majanga mengine ya Asili.
Bima ya Nyumba inajumuisha Vitu gani?
Bima ya Nyumba itakulinda katika sehemu kuu zifuatazo utakazokatia;Bima ya Mali itajumuisha;
- Vitu vyote vya thamani vilivyomo ndani ya nyumba au jengo la Biashara.
- Mali zinginezo kama simu, kamera, saa, cheni, mabegi, vinakilishi, Kompyuta, n.k.
USINGOJEE MAJANGA YATOKEE NDIO UKATIE BIMA MALI ZAKO EWE MFANYABIASHARA.
Gharama ya Bima ya Nyumba ni kiasi gani?
Bima ya nyumba ni gharama nafuu sana na inalipwa mara moja kwa mwaka kuzingatia vitu mbalimbali vitakavyobainishwa muda wa kukatia.Ada ndogo
(Premium) kabisa kwa mwaka ni Tshs 59,000 kwa nyumba yenye thamani ya Tshs
35,000,000# na itakuwa ikiongezeka kadri thamani ya nyumba inavyoongezeka, kwa
mfano;
Ada ya Bima
ni 0.15% ya thamani ya nyumba yako, Bima zote za mali huchajiwa kodi hivyo
utalipia kodi (VAT) ya 18%.
Thamani ya Nyuma (Tshs) |
Ada kwa Mwaka (Tshs) |
35,000,000 |
61,950 |
50,000,000 |
88,500 |
75,000,000 |
132,750 |
100,000,000 |
177,000 |
150,000,000 |
265,500 |
200,000,000 |
354,000 |
Nahitaji vitu gani vya muhimu ili nikatie Nyumba au Mali Bima?
Hakikisha
una kielelezo chochote kile kinachoonesha kuwa wewe ndio mmiliki halal wa
nyumba, mfano; Hati ya Nyumba, Bili ya Maji au Malipo ya Luku, Mauziano ya
Kijiji, Stakabadhi ya Malipo ya Ardhi, n.k.
Ili kukatia Malizako tutahitaji yafuatayo:
-Kitambulisho chako.
-Mkataba wa Kupanga eneo la biashara / nyumba
-Tutakutembelea na Kupiga Picha ofisi kwa wafanyabiashara.
EWE MFANYABIASHARA TUNAKUSHAURI UKATIE BIMA MALI ZAKO.
Wasiliana na
sisi sasa hivi:
Namba za simu: +255 754 233 717
Email: tzcovenant@gmail.com / elinsuranceltd@gmail.com
0 comments:
Post a Comment